MWONGOZO WA MALIPO YA ADANA MICHANGO MINGINE

MWONGOZO WA MALIPO YA ADA
NA MICHANGO MINGINE

 

Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Nyaishozi kama ilivyo kwa vyuo vyote hapa Tanzania, ada ni kigezo cha kwanza cha kumtambulisha mwanafunzi halali wa Chuo husika. 

 

Sera ya Chuo cha Afya Nyaishozi inamtambua mwanafunzi ambaye amekamilisha ada na michango Mingine kwa asilimia mia moja (100%) kama mwanafunzi halali anayestahili haki zote kama Mwanafunzi. Hivyo Wanafunzi hupokelewa baada ya kukamilisha Ada na Michango mingine.

 

Ikumbukwe kuwa Ada (Tuition Fees) ndizo zimegawanyika mara mbili kwa semesta. Michango Mingine inalipwa mwanzoni mwa Mhula kwa ujumla wake na hairejeshwi.

 

Kutokana na hali ya uchumi wa Wazazi au Walezi wa Wanafunzi wetu, Chuo kinaweza kutoa ahueni kwa mwanafunzi kulipa ada na michango Mingine kwa awamu. Ikumbukwe kuwa mwaka wa masomo huanza Septemba hadi Augosti ya mwaka unaofuata. Kimasomo, mwaka wa masomo una mihula miwili. Aidha mwaka wa Masomo kimasomo una miezi ya kalenda 10, ambazo ni sawa na wiki 40 za masomo na miezi miwili ya mapumziko. 

 

Kwa mantiki hiyo, Mwanafunzi ambaye hana uwezo wa kulipa Ada na Michango Mingine, ataruhusiwa kwa kuwasilisha maombi ya ulipaji wa Ada na Michango Mingine kwa awamu. Endapo Utawala wa Chuo utaona inafaa, ataruhusiwa kulipa kwa awamu.

 

Ulipaji wa awamu upo katika makundi matatu yafuatayo:-

 

  1. Kulipa kwa awamu mbili – Mwanafunzi husika ataruhusiwa kulipa asilimia hamsini (50%) ya ada na michango mingine mwanzo wa semesta ya kwanza na asilimia hamsini zilizobaki mwanzo wa semesta ya pili. 

     

    Kwa mfano kama Ada na Michango Mingine ni TShs 2,200,000; Mwanafunzi ataruhusiwa kulipa 1,100,000/= mwanzo wa Semesta ya kwanza, na kiasi kilichosalia atalipa mwanzo wa semesta ya pili.

     

  2. Kulipa kwa awamu nne – Mwanafunzi husika ataruhusiwa kulipa asilimia ishirini na tano (25%) ya ada na michango Mingine, mwanzo wa semesta ya kwanza; Asilimia 25 mwisho wa mwezi wa December. Asilimia 25 Mwanzo wa semesta ya pili na Asilimia 25 katikati ya Semesta ya pili. 

     

    Malipo yatakuwa kama ifuatavyo:-
    1. September (25%)
    2. December (25%)
    3. March (25%)
    4. June (25%)

     

    Kwa mfano kama ada na Michango Mingine ni TShs 2,200,000; mwanafunzi atalipa 550,000/=  mwanzo wa semesta ya kwanza (September). Atalipa 550,000/= katikati ya semesta ya kwanza (December); atalipa 550,000/= mwanzo wa semesta ya pili (March); na kumalizia 550,000/= katikati ya semesta ya pili (June).

     

  3. Kulipa kwa kila mwezi – Mwanafunzi anaruhusiwa kulipa kila mwezi asilimia 10 ya jumla ya Ada na Michango Mingine kuanzia September. Malipo yafanyike mwisho wa mwezi bila kuruka mwezi.
    1. September (10%)
    2. October (10%)
    3. November (10%)
    4. December (10%)
    5. January (10%)
    6. February (10%)
    7. March (10%)
    8. April (10%)
    9. May (10%)
    10. June (10%)

    Kwa muktadha huo, tukitumia mfano wa ada na Michango Mingine ni TShs 2,200,000; hapo juu; mwanafunzi atatakiwa kulipa 220,000/= kila mwezi kuanzia September. 

 

ANGALIZO

  • Mwanafunzi ambaye atakiuka utaratibu huu wa malipo, hataruhusiwa kushiriki katika vipengele vikuu vya masomo katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Nyaishozi kama kufanya CAT, kuhudhuria mafunzo kwa vitendo nk
  • Mwanafunzi atakayekatiza masomo lazima ahakikishe amelipa michango yote na ada (Tuition Fees) ya semesta aliyomo. 
  • Wanafunzi wanaorudia Semesta au moduli lazima walipe michango yote Pamoja na ada (Tuition Fees) ya semesta husika.
  • Mwanafunzi anayehama, ahakikishe amelipa michango yote na ada ya semesta husika ili aruhusiwe kuhama.
MICHANGO MINGINE