- Wanafunzi wote wanatakiwa kujisajili katika kitabu maalum cha hosteli siku ya kuripoti hosteli.
- Usafi wa ndani ya chumba utafanywa na wanafunzi wanaoishi ndani ya chumba hicho.
- Usafi wa choo utafanywa na wanafunzi watakaotumia vyoo hivyo.
- Gharama za umeme katika chumba zitagharamiwa na wanafunzi watakaokuwa wanatumia chumba husika.
- Gharama ya maji na takataka zitahusisha wanafunzi wote wanaoishi katika hosteli kwa ujumla wao.
- Ni marufuku kutumia jiko la aina yeyote ndani ya hosteli. Mwanafunzi atakayepatikana na vifaa vyovyote vile vya kupikia atafukunzwa kuishi ndani ya hosteli na vifaa hivyo kuchukuliwa. Faini itatozwa kwa atakayekutwa na vifaa hivyo.
- Ni marufuku kupiga kelele, kufungulia redio kwa sauti kubwa, kutumia lugha ya matusi/chafu,kupigana na vitendo vingine kama hivyo katika hosteli. Mwanafunzi atakayepatikana na makosa yaliyotajwa hapo atakuwa amepoteza sifa ya kuishi hosteli.
- Wageni HAWARUHUSIWI kuingia ndani ya hostel; kwa yeyote atakayevunja sheria atakuwa amepoteza sifa za kuishi hosteli hivyo atafukuzwa mara moja.
- Mwisho wa kuingia ndani ya hosteli ni saa 2 usiku na mlango wa geti kuu utafungwa wakati huo.
- Ulinzi wa vifaa katika hosteli ni jukumu la wanafunzi wanaoishi hosteli.
- Muda wa kuondoka hosteli kuelekea chuo ni kuanzia saa 12 kamili asubuhi hadi saa 1 kamili asubuhi kwa kutumia basi la chuo.
- Mwanafunzi haruhusiwi kula chakula kilichoandaliwa nje ya Chuo kwa ajili ya usalama.
KUMBUKA
- Wizi, uasherati, ulevi, kupigana, matusi, utumiaji wa madawa ya kulevya,uvutaji wa sigara na matendo machafu yatakufanya UFUKUZWE CHUO.
- Hairuhusiwi mwanafunzi kuishi na mke/mume au mototo ndani ya hosteli za chuo. Ukigundulika adhabu ni kufukuzwa kuishi katika hosteli.
- Uongozi una hiari ya kufanya ukaguzi wakati wote katika vyumba vya hosteli.